Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Rukwa, Eng. Grace Chitanda akisaini mkataba wa makabidhiano ya kifaa cha kupimia wingi wa maji mtoni, pamoja na kifaa cha kupima ubora wa maji. Vifaa hivi vimetolewa na shirika la maendeleo la Uholanzi SNV, chini ya mradi wa IKI Katuma unaosimamiwa na shirika la maendeleo la Ujerumani GIZ. Mradi huu unaoendelea katika kidakio cha Katuma, unalenga kusimamia Bioanuwai kwa kutumia usimamizi shirikishi wa Rasilimali za Maji.